Wananchi waanza kupimiwa ardhi
Serikali imeanza kuchukua hatua ya kurasimisha ardhi na nyumba za wakulima na wafugaji ili kuwawezesha kupata mikopo benki, mifuko na taasisi za fedha nchini ili kuwaondoa katika umaskini uliokithiri.
Kauli hiyo ilitolewa juzi na Waziri wa ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, John Chiligati wakati akizindua upimaji na utoaji wa hati miliki za ardhi kimila uliofanyika Wilaya ya Bariadi mkoani Shinyanga.
Wilaya hiyo ni moja ya maeneo ya majaribio kitaifa. Nyingine ni ya Babati mkoani Arusha pia.
Uzinduzi huo wa mpango umefanyika baada ya viongozi wa serikali na vyama vya kisiasa na wataalamu kupewa mafunzo elekezi wilayani humo ya kuchambua chimbuko la mradi huo katika utekelezaji wa sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995 na Sheria ya Ardhi ya Vijiji namba 5 ya mwaka 2004.
Chiligati alisema hatua hiyo ni ya utekelezaji wa Mkakati wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara Tanzania (Mkurabita) kwa lengo la kuwawezesha Watanzania kurasimisha ardhi na nyumba zao ili waweze kuzitumia kupata mikopo kwa urahisi.
Alisema mpango huo ambao ni wa kwanza kutekelezwa nchini utawawezesha wakulima na wafugaji kumiliki ardhi zao za kimila kwa kuhusisha serikali za vijiji na kupanga matumizi bora ya ardhi.
Alisema maeneo muhimu ambayo yatazingatiwa wakati wa upimaji huo ni ya makazi, huduma za kijamii, makaburi na maeneo ya hifadhi ya ardhi ya kijiji kama vile maeneo ya malisho.
Alisema baada ya kutambua kila kipande cha ardhi ndani ya kijiji chini ya mpango huo, ndipo utekelezaji utafanyika kwa kutambua mipaka ya kila mwenye shamba au eneo la malisho ya mifugo na kuweka mipaka bayana.
Pamoja na kuweka kumbukumbu za miliki ya ardhi bayana, alisema mpango huo pia utammilikisha na kumpatia kila mhusika hatimiliki ya eneo lake, wakati kipande cha ardhi kwa mtu mmoja mmoja au familia ya mume na mke au eneo linalomilikiwa kiukoo itamilikishwa kwa kupitia kiongozi wa familia au ukoo.
Chiligati aliagiza kuwapo kwa ushirikishwaji wa kila mwanakijiji na kuutaja mradi huo kuwa ni shirikishi.
SOURCE: Nipashe, 2009-03-03 10:55:06
Na Stephen Wang`anyi, Shinyanga
Showing posts with label Arusha. Show all posts
Showing posts with label Arusha. Show all posts
Tuesday, 3 March 2009
Tuesday, 20 January 2009
Simu ya Polisi Arusha
Polisi Arusha watoa namba mpya kudhibiti uhalifu
Wakazi wa Arusha wametakiwa kutumia simu namba
0767 750173,
kutoa taarifa za dharura kwa jeshi la Polisi Mkoani humo iwapo kutatokeaa tatizo lolote la uhalifu katika eneo husika.
Akiongea na vyombo vya habari ofisini kwake, Kaimu Kamanda wa Polisi,Mkoa wa Arusha, Roberti Boaz, alisema kuwa, simu hiyo ni maalum kwakutumia ujumbe wa maneno kwa gharama nafuu.
"lengo la kutoa namba hii, kurahisisha utoaji wa taarifa kwa wananchi,wengine wanapata tukio ila wanashindwa kuja polisi kwa umbali, lakinikwa kutumia simu itasaidia kushirikiana" alisema Boaz
(chanzo: Faustine's Baraza)

Labels:
Arusha,
Mambo ya Ndani,
Tanzania,
Ulinzi na Usalama
Subscribe to:
Posts (Atom)