Tuesday, 17 March 2009

Tunahitaji Kituo Kikubwa cha Basi Mbagala Rangi Tatu

Hii ni kwa wakazi wa Mbagala peke yao...

Wazo hili nimeliandika kwa ajili ya gazeti la serikali la HabariLeo la Jumatatu 16/03/2009


Kwa hili madiwani wa Temeke mmechemsha

BARABARA ya Kilwa ambayo imejengwa njia mbili inakaribia kumalizika huku kituo cha mabasi kikubwa katika barabara hiyo cha Mbagala Rangi tatu kikiwa hakina mwelekeo wowote ule wa msingi.

Tetesi ambazo zinazunguka katika maeneo hayo ya Mbagala Rangi tatu na hii nadhani ni kweli, madiwani wa Temeke na wataalamu wao wameamua mahali lililopo soko katika eneo hilo ndiko kunakofaa kuwa na kituo cha mabasi.

Wakati fulani unashangaa uwezo na busara za watu katika kufanya mipango miji na maendeleo yake hasa kwa kuzingatia ukuaji wa mji na pia maeneo yanayozunguka mji wenyewe.

Lakini kwa mawazo yangu mimi busara, akili katika hili haikufuatwa, bali tamaa ndiyo ilitangulizwa mbele katika maamuzi haya ambayo kimsingi mimi nayaona kama yamejaa ubabaishaji.

Kwa eneo kama la Rangi Tatu ambalo kwa sasa linapokea magari yote ambayo yanatoka mpaka mkoa wa jirani wa Pwani ukiachia mbali mabasi yanayotoka maeneo mbalimbali ndani ya Mbagala yenyewe ambayo ni kubwa kama wilaya kubadili soko kuwa kituo cha mabasi ni dalili ya ufidhuli wa akili, na hili si tusi.

Nasema si tusi kwa sababu miaka mitano ijayo Mbagala Rangi tatu itapokea magari mengi kutoka katika wilaya inayokuja kwa kasi kwa shughuli mbalimbali za kiuchumi ya Mkuranga.

Ukiangalia pia mipango ya serikali kuu kuhusiana na Mkuranga na wazo la kujenga moja ya viwanja vikubwa vya ndege nchini, mtu ataiangalia Mbagala Rangi tatu kama sehemu inayohitaji Bus terminal na wala si Bus Stop.

Nasema ni Bus Terminal wala si Bus Stop kwa sababu mazingira yanaonyesha wazi kuwa panahitajika eneo kubwa la mazingira ya bus Terminal kama inavyostahili kuwa na katika hili eneo la soko ni eneo si tu dogo bali la kulazimisha.

Mbagala Rangi tatu ina sehemu kubwa ya kuweza kujenga Bus Terminal ambayo inaweza kuchukua mabasi ya kawaida hata mia nane ikiwa na ukubwa sawa na Ubungo Bus Terminal na ipo sehemu nzuri tu ambapo kuingiza na kutoa mabasi hakuhitaji ufundi mkubwa.

Eneo hilo ambalo wajanja walishataka kuliuza kwa milioni 800/- awali tunaambiwa lilikuwa ni miliki ya UDA kama ilivyokuwa Ubungo. Sehemu hii wapo wajanja wengi wameikomalia kama yaop na wanataka kuifanyia kazi ambayo ni ya kijanja zaidi.
Eneo hili ambalo lipo mkabala na Kanisa la Kristo,mbele ya Shule ya kimataifa ya St Mary's ni ardhi ambayo bado haijaendelerzwa sana na ingeliweza kufaa kuwa terminal na pia kitega uchumi bora kabisa kwa wilaya ya temeke ambayo inasuasua katika vitega uchumi vyake.

Lakini madiwani na mkurugenzi wake wameamua kuchukua mahali ambapo mimi napaona padogo na pia kuleta usumbufu kwa watu waliopo pale bila sababu na kisha unatazama watu wataingizaje mabasi yao na kuyatoa.

mathalani watu wanaokwenda Kiburugwa njia ya awali ambayo imefikiriwa kutumiwa kuingiza mabasi stendi hiyo inayofikiriwa,(sokoni) inapita karibu kabisa na njia ya bomba la mafuta na ukweli huu unatisha. Nasema unatisha kwa sababu hakuna mtu anayetaka kuukubali ukweli kuw abarabara ile iko katika eneo lilisloruhusiwa na tumefumbia macho.

Pili kutahitaji ubunifu wenye gharama kubwa kuzungusha mabasi katika eneo hilo na kuingia katika barabara kuu wakati kwa kutengeneza terminal mbele ya st Marys eneo hilo linalodaiwa kuwa la UDA kuingia katika eneo hilo ni rahisi na kutoka kwani ni kama muonmdoko wa sambusa.

Nini kinawapeleka madiwani na wapanga miji kufikiria leo badala ya kufikiria kesho na kesho kutwa, mimi sijaelewa. Na kwa kuwa sheria ya ardhi inatoa mamlaka makubwa kwa serikali kubadili matumizi kw akuzingatia hali halisi ya sasa na ijayo na ili tusije tena kubomoa eneo hili ambalo wajanja wanataka kuliuza kwa milioni 800/- linafaa kujengwa kituo na kumaliza uzia.

Mimi sielewi kama kweli tunahitaji fundi kutoka mbinguni kutuambia kwamba pale sokoni hapatufai kwani na mtu akinunua kiwanda cha biasi itakuwaje hasa? Kiwanda hiki ingawa hakitumiki kwa sasa kilijengwa kwa ajili ya kutengeneza kioo.

Mimi naamini historia itakuja kutusuta kwa mara nyingine tena, baada ya makosa mengi katika mipango miji yetu na hili la Mbagala Rangi tatu litakuwa jingine tena ndani ya vurumai za kuendekeza 'mkato' badala ya ukweli wa maslahi ya umma.

Je tunahitaji tena kupelekwa shule kujua kwamba tunatakiwa kutumia akili zetu kwa kuangalia mbele zaidi na wala si leo, au kila Rais akiingia madarakani aje na dizaini ya bomoa hapa kwani tumekosea pale?

Nini hasa maana ya kuwa na madiwani na maafisa mipango wasioangalia ukweli kwa kutumia akili yao na kusikiliza ushauri kwa waliokuwapo.
mwisho


posted by Msimbe @ 10:18 PM

source: lukwangule.blogspot.com

Commonwealth

The English noun commonwealth dates from the fifteenth century. The original phrase "common-wealth" or "the common weal" comes from the old meaning of "wealth," which is "well-being." The term literally meant "common well-being." Thus commonwealth originally meant a state or nation-state governed for the common good as opposed to an authoritarian state governed for the benefit of a given class of owners. Commonwealth derives from the Latin term res publica, a broad concept which is also sometimes translated as "public affairs" or "the state" in certain contexts. Res publica is also the term from which the English word republic arises.

Today the term is more general and means a political community.

The type of community indicated by the term commonwealth varies. For instance, in different contexts it might indicate:

a political unit founded in law by agreement of the people for the common good;
a federated union of constituent states;
a community of sovereign states;
a republic;
a democratic constitutional monarchy;
When capitalized, "Commonwealth" normally refers to the 53 member Commonwealth of Nations


(From Wikipedia, the free encyclopedia)

Monday, 16 March 2009

Lawama: utoaji wa hatimiliki za viwanja TZ

Ufisadi watikisa Ardhi

Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi imetupiwa tuhuma nzito za ufisadi katika suala zima la utoaji wa hatimiliki za viwanja.

Tuhuma hizo zimetolewa na wananchi mbalimbali ambao wanadai kwa muda mrefu sasa wamekuwa wakihangaikia bila ya mafanikio kupata hati za miliki za viwanja vyao ambazo hutolewa na wizara hiyo.

Wizara hiyo inalaumiwa kuwa na urasimu mkubwa katika utoaji wa hati hizo kiasi cha kusababisha waombaji wakae muda mrefu bila ya kuzipata na wakati mwingine kulazimika kutoa rushwa kwa baadhi ya maafisa wake wasio waaminifu ili waweze kuzipata kirahisi.

Wakizungumza na Nipashe Jumapili kwa nyakati tofauti kuhusiana na suala hilo, baadhi ya wananchi wameilalamikia Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi, kuwa imekuwa ikiwazungusha kwa muda mrefu katika kuwapatia hati za viwanja vyao pamoja na kwamba wamekamilisha taratibu zote zinazotakiwa.

Wananchi hao wamelalamika kuwa kutokana na kucheleshwa kupata hati hizo kwa sababu zisizojulikana, wamekwama kufanya shughuli zao mbalimbali za maendeleo zinazohusiana na viwanja hivyo kama vile kuviendeleza au kutumia hati hizo kuomba mikopo benki kwa ajili ya kupambana na umasikini.

Mmoja wa wananchi hao kutoka mkoani Arusha ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini, alidai amekuwa akizungushwa kwa muda wa miezi mitano sasa kupata hati ya shamba lake, hali ambayo alidai imekwamisha mipango yake mingi ya kukiendeleza kiwanja hicho pamoja na kuitumia hati hiyo kuomba mkopo benki.

Alisema yeye ni mmoja wa watu waliohamasika na mpango wa serikali wa kuwapatia wananchi hati miliki za maeneo yao baada ya kuyapima ili waweze kuomba mikopo benki kwa ajili ya kupambana na umasikini, lakini Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi inamkatisha tamaa kutokana na utaratibu wake usioeleweka wa kutoa hati hizo.

``Serikali inatuhamasisha wananchi kupima maeneo yetu ili tupewe hati za umiliki zitakazotuwezesha kukopa benki, sasa tunashangazwa na wizara hii ambayo ndiyo yenye jukumu la kutoa hati hizo kutuzungusha kwa muda mrefu na wala hatujui tatizo ni nini maana hatujibiwi chochote,`` alisema.

Alifafanua kuwa yeye pamoja na wenzake wengine ambao nao wanakabiliwa na tatizo kama hilo, wametimiza taratibu zote za kupatiwa hati hizo kuanzia ngazi ya kijiji hadi kanda ambako ndiko hati hizo inakotolewa, lakini wameelezwa kuwa kanda haina mamlaka ya kuzitoa na kwamba zimetumwa wizarani Dar es Salaam ambako zimekwama huko wao wakisubiri kwa muda mrefu bila ya wao kujua kinachoendelea.

``Kwa utaratibu mtu anatakiwa kuanzia ngazi ya kijiji kwa kuitisha mkutano wa wanakijijiji wakikubali unaenda wilayani ambako unapewa kibali cha kupima ardhi kabla ya kwenda ngazi ya mkoa na kisha kanda ambako hati husajiliwa na kutiwa saini, mimi nimetimiza yote hayo lakini nilipoenda ofisi ya kanda nikaambiwa zimepelekwa wizarani ambako zimekwama,`` alieleza.

Nipashe Jumapili lilipowasilliana kwa njia ya simu na Kamishna wa Ardhi Kanda ya Kaskazini ili kujua ni tatizo gani linalosababisha kuchelewa kutolewa kwa hati hizo kufuatia malalamiko ya baadhi ya wananchi alikataa kutoa ushirikiano na badala yake ilitaka wizara ndiyo iulizwe kuhusiana na suala hilo.

Malalamiko kama hayo pia yametolewa na baadhi ya wananchi jijini Dar es Salaam na kutoka mikoa mingine, kuwa inawachukuwa muda mrefu sana kupata hati za umiliki wa maeneo yao huku wakiwa hawajui tatizo ni nini pamoja na kufuata taratibu zote zinazotakiwa.

Wananchi hao wamemuomba Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, John Chiligati, kulifuatilia kwa karibu tatizo hilo ili kulipatia ufumbuzi wa haraka, kwa kile walichodai kuwa baadhi ya maafisa wa wizara hiyo siyo waaminifu kwani wamekuwa wakifanya makusudi kuchelewesha kutoa hati ili waweze kupewa rushwa.

Walisema wizara hiyo inatakiwa kwenda sambamba na kauli mbiu ya Rais Jakaya Kikwete ya Ari Mpya, Nguvu Mpya na Kasi mpya katika utendaji wake ikiwa ni pamoja na kuwaondoa watumishi wote wanaokwenda kinyume na maadili ya kazi zao ili kuleta ufanisi.

Nipashe Jumapili lilipowasiliana na Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, John Chiligati, kuhusiana na malalamiko hayo ya wananchi alionekana kushangazwa na maelezo hayo, akieleza kuwa kwa sasa hakuna tatizo kama hilo la ucheleweshaji wa utoaji wa hati za umiliki wa ardhi.

Alieleza kuwa tatizo hilo lilikuwapo zamani lakini wizara yake imeshalifanyia kazi na kwamba kwa sasa halipo tena, tofauti na madai ya wananchi hao.

Chiligati, alifafanua kuwa kutokana na tatizo hilo kuwa sugu siku za nyuma, wizara yake ilianzisha utaratibu wa maombi ya hati za umiliki wa ardhi kushughulikiwa katika kanda badala ya wizarani, ili kuwawezesha wananchi kuzipata bila ya usumbufu na kwa haraka.

``Tatizo hilo limekuwa historia, tangu tupate uhuru maombi yote yalikuwa yanashughulikiwa wizarani tu na Kamishana wa Ardhi, lakini sasa tumeunda kanda tano kwa ajili ya kurahisisha mambo, mimi ndiyo muasisi wa utaratibu huu, wananchi wanatakiwa kupeleka maombi yao huko kwa ajili ya kupatiwa hati za umiliki wa ardhi badala ya kuja moja kwa moja wizarani kama zamani,`` alifafanua.

Alizitaka kanda hizo kuwa ni Kanda ya Kaskazini, Kanda ya Ziwa, Kanda ya Kusini, Kanda ya Kati na Kanda ya Mashariki.

Alitoa wito kwa mwananchi yoyote anayezungushwa kupata hati hizo baada ya kukamilisha taratibu zote aende wizarani akaonane naye ili aweze kushughulikia tatizo hilo.

Kwa muda mrefu sasa kumekuwa na malalamiko mengi kutoka wananchi wakiilalamikia baadhi ya maofisa wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi kuwa wamekuwa kikwazo katika utoaji wa hati za umiliki wa ardhi kwa lengo la kupewa rushwa, hali ambayo inakwamisha mipango yao ya kuboresha hali zao za maisha.


SOURCE: Nipashe, 2009-03-15 14:08:05
Na Abdallah Bawazir

Friday, 13 March 2009

Hunger in TZ

Over 240,000 people face hunger

More than 240,000 people in Tanzania are in urgent need of food aid, while 12,000 others will have to get the food at a subsidised price as the growing food crisis takes its toll in some regions.

Agriculture, Food Security and Cooperatives minister Steven Wassira said in Dar es Salaam yesterday that this was the latest information he had received from the team of experts the government dispatched to evaluate the extent of food crisis in 13 regions.

The minister briefed reporters on the food situation at a ceremony at which a memorandum of understanding was signed on development assistance to Tanzania`s agricultural sector between China Development Bank (CDB) and his ministry.

He said the food aid the government would dispatch to the food-short regions would be given for free to those who cannot afford even the token price, while others would have to buy it at a subsidised price.

``Preliminary reports brought to me by the team of experts show that over 240,000 people deserve food aid because they cannot pay for it, while 12,000 others can buy it at a token price,`` he elaborated.

The minister said, as a precaution, the government was making sure that food was not taken to neighbouring countries.

He noted that Kenya and Zimbabwe were already facing food shortages and expressed fears that the situation in Tanzania could worsen ``if people continue taking food across our borders despite the standing ban``.

``The government has taken enough measures to make sure that people do not export or otherwise take foodstuffs to neighbouring countries because it will worsen the crisis in the country,`` he said.

``The team of experts is helping in assessing the country`s actual food needs and the extent to which food aid will be required. It has already left for the food-short regions for the purpose,`` explained Wassira.

He named the regions as including Arusha, Dodoma, Iringa, Kagera (Bukoba), Kigoma, Kilimanjaro (Same), Lindi, Mara, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Shinyanga and Tanga.

He would not give details on the degree of the problem in each region.

The government last week allayed public fears over reports of looming famine in the 13 regions.

Agriculture, Food Security and Cooperatives deputy minister David Mathayo told this paper that the team of experts earlier sent to 11 regions most hit by food shortages reported that the situation was not as severe as earlier thought and that there was no cause for alarm.

CDB chairman Zheng Qingh, who represented his bank at yesterday`s ceremony, said the package would help Tanzania improve its agriculture.

He said the package would enable farmers to improve farming methods and produce enough food for both domestic use and sale.


SOURCE: Guardian, 2009-03-12 10:55:37
By Angel Navuri

Tuesday, 10 March 2009

'Umependa Ua, Boga Lake Je?'

.
.
Anakupenda ukiwa na mumeo, lakini ukiachwa yeye anakutosa

Mpenzi msomaji, wapo watu wengine aibu kwao ni mwiko. Kazi yao ni kama golikipa anayesubiri mpira golini ili audake au auteme kama mambo yakiwa magumu.

Naam. Ipo tabia moja ambayo imekuwepo kwa muda sasa ndani ya jamii yetu na inatesa baadhi ya familia lakini wahusika wanagumia maumivu kimya kimya wasijue cha kufanya.

Eti bila haya wala huruma ya kibinadamu unamendea cha mwenzio na kukorofisha ndoa yake au unyumba wake, lakini bibie akiachwa kwa ajili yako, nawe unamtosa. Ebo!

Tabia hii naweza kuitolea mifano katika sura mbili tofauti. Sura ya kwanza ni wale wanaume mafedhuli, tena wenye ndoa zao wanapodiriki kuwarubuni wake za wenzao na kujenga mahusiano, lakini pindi wenye wake wanapong`amua na kuwaacha, nao pia wanawatosa. Si unajua tena mshika mawili moja humponyoka? Mimi naongezea kuwa mshika mawili pia yote yaweza kumponyoka.

Sura ya pili ni ile mijamaa inayomezea wake za wanaume wenzao na pindi mahusiano hayo yanapogundulika, basi dowezi yule huamua kumchukua mke yule jumla jumla.

Yaani unasubiri mwenzio achague mchuchu wake, achombeze gharama kibao na hata amzalie mtoto au watoto, kisha wewe ujichukulie kiulaini? Hawa hawamuogopi Mungu anayekemea kutotamani cha mwenzako ikiwa ni pamoja na mke? Ama kwa hakika Maisha Ndivyo Yalivyo.

Katika sura ile ya kwanza hebu nikupe mfano mmoja ninaokumbuka uliotokea hapa jijini miaka ya nyuma. Yupo mama mmoja aliyekuwa na ndoa yake imara na alibahatika kuzaa watoto wake wawili.

Mumewe aliheshimu sana ndoa yake na hata kama alikuwa akichepuka kusaka vidosho alifanya kwa siri sana.

Mkewe kwa kuchukulia upole wa mumewe, tamaa zikamfanya avunje uaminifu na katika pilikapilika zake akampata mtaalamu mmoja mzungu aliyekuwa nchini kikazi. Kwa siri mzungu huyu akamjengea nyumba mama huyu.

Aliimarisha mahusiano hayo kwa siri hata akapata ujauzito wa mzungu. Hali hiyo ilimfanya wakati mwingine ajisahau na kutorudi nyumbani. Akiulizwa anatoa sababu zilizotia shaka.

Hata hivyo, akatafuta mazingira ya kumkorofisha mumewe na hapo akatoweka nyumbani kabisa. Mume alipochunguza akagundua kuwa amewekwa kinyumba na mtaalamu huyo wa kizungu.

Ilibidi mume apate ushauri toka kwa washenga, wazee wa koo za pande zote mbili. Mke akaitwa kwenye kikao akakataa. Mume huyu akaamua kuvuta pumzi aone mwisho wa mama huyu.

Ilifikia wakati mzungu yule akamuuliza mwanamama huyu mbona haendi nyumbani kuona familia yake, lakini naye akawa anamvunga kuwa imehamia mikoani ndio sababu yuko naye wakati wote.

Nyumba ikawa imekamilika na mzungu na bibie wakahamia na siku chache baadaye akajifungua mtoto chotara. Mzungu hakutaka azae mtoto na mama yule hasa kwa kutambua kuwa alikuwa mke wa mtu.

Alipoona mtoto mzungu ikabidi atafute mazingira ya kumtoroka bibie.

Siku moja bibie alitoka kwenda kwa jamaa zake na ndipo mzungu akapata mwanya wa kuishia zake. Pengine ni kwa kuhofia kushtakiwa kwa kuvuruga ndoa ya mwanaume mwenzie.

Bibie kurudi akagundua kuwa mzungu alishachukua vitu vyake vyote muhimu na alipochunguza kazini akajibiwa kuwa alishaondoka zake kurudi ulaya.

Mama huyu akabaki ameduwaa asijue la kufanya. Kwa mume hawezi kurudi hasa baada ya kuzaa nje ya ndoa.

Katika sura ya pili, yupo mwanamama mmoja ambaye naye alikuwa na ndoa yake imara huku wakijaliwa kupata watoto watatu. Lakini kwa tamaa zake, akaivunja mwenyewe na sasa yupo yupo tu.

Mumewe alikuwa mtumishi wa umma mwenye madaraka. Walikuwa wamejenga nyumba yao nzuri, watoto wanne na mtoto wao mkubwa tayari amemaliza chuo.

Bibie huyu pamoja na kutunzwa vema huku akiwa na shughuli zake za ujasiriamali, lakini bado aliruhusu mahusiano ya nje na bosi mmoja mwenye cheo serikalini.

Ni bosi mwenye mke na watoto kibao, tena kwa wanawake tofauti. Mahusiano haya yakawa moto.

Wapambe wa mume huyu wakamtaarifu nyendo za mkewe na bosi yule. Mume bila taharuki akachunguza kwa muda.

Hatimaye aliwafuma wakiwa ndani ya gari na alipoulizwa akajitetea kuwa ilikuwa ni lifti.

Hata hivyo, jamaa akatafuta watu wawili ambao walikuwa wakimuona bibie na kibosile yule na kutoa ushahidi, tena mbele ya washenga.

Mume huyu hadi leo hajatoa talaka lakini aliamua kutengena na mkewe na tayari ameshaoa mke mwingine. Bibie naye akaona kuliko akose kote afadhali amuegemee kibosile yule.

Kwa sasa amepangishiwa nyumba na amekuwa mmoja wa wake wadogo wa bosi yule. Swali ni je, vituko vya aina hii vina tija gani katika maisha haya?

Yafaa kinamama na kinababa wajiulize migongano ya aina hii ya kimahusiano yanayobomoa nyumba zao, nini basi kifanyike?

Una mke au mume mzuri ambaye ulimchangua mwenyewe, sasa hizi tamaa za fisi zinatoka wapi? Hata kama utasema chaguo lile halikuwa lako au ulikosema kuchagua, sasa kwanini uopoe wa mwenzio? Huu ni wizi mtupu, tena wa mchana kweupe.

Tabia hii ya kutamani vya wengine imevuruga nyumba zetu nyingi. Yafaa watu wabadilike, hasa kwa kuzingatia` kuwa tabia hii imechangia sana kuenea kwa maambukizi ya virusi vya ukimwi, ongezeko la watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi kutokana na ama wazazi kuachana. Kutengana au hata kufa.

Ulaghai wa baadhi ya kinababa nao siachi kuukemea kwani umechangia baadhi ya kinamama kuhadaika kwa kununuliwa magari, kujengewa nyumba na hata kuanzishiwa miradi ya kibiashara na watu wengine nje ya ndoa zao.

Binafsi naona ni mateso ya kiroho wanayopata wale wote waliojikuta kwenye mtego inayohusiana na mifano niliyotaja na mengineyo.

Zaidi pia ni majuto kwani walioharibu nyumba zao wenyewe, bila shaka wanazitamani tena lakini inashindikana. Si unajua maji yakimwagika hayazoleki?

Naam. Mpenzi msomaji niishie hapa nikupe fursa nawe uchangie ili sote kwa pamoja tuelimishane na jamii yetu kwa jumla. Ukiwa nayo maoni, hata jambo linalokukera kuhusu maisha ndani ya familia zetu, nikandamizie kupitia:

fwingia@yahoo.com
Wasalaam.


SOURCE: Nipashe, 2009-03-08 11:35:45
Na Anti Flora Wingia

Friday, 6 March 2009

Hotuba ya Mhe Rais Kikwete (Jeshini)

HOTUBA YA MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA AMIRI JESHI MKUU WA JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA, KWENYE UZINDUZI WA KAMANDI YA JESHI LA NCHI KAVU YA JESHI LA ULINZI WA
WANANCHI WA TANZANIA, MSANGANI, PWANI,
TAREHE 04 FEBRUARI, 2009

Mheshimiwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la
Kujenga Taifa;
Mheshimiwa Naibu Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya Ufundi;
Mheshimiwa Mkuu wa Majeshi;
Mnadhimu Mkuu wa Jeshi;
Mheshimiwa Katibu Mkuu;
Waheshimiwa Viongozi wa Serikali;
Wakuu wa Majeshi Wastaafu; Wanadhimu Wakuu
Wastaafu na Majenerali Wastaafu
Kamanda Kamandi ya Nchi Kavu;
Ndugu Makamanda na Wapiganaji;
Wageni Waalikwa;
Mabibi na Mabwana.

Napenda kuanza kwa kutoa shukrani zangu za dhati kwa heshima mliyonipa ya kunishirikisha kwenye sherehe hii adhimu ya uzinduzi wa Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania. Kunishirikisha kwenu kwenye tukio hili muhimu kunanipa faraja kubwa kwani nami ninakuwa sehemu muhimu ya historia ya maendeleo ya Jeshi letu.
Waheshimiwa Mawaziri, Makamanda na Wapiganaji;
Siku ya leo ni siku muhimu sana katika historia ya jeshi letu. Ni siku ambayo tunashuhudia mabadiliko ya muundo wa kiutawala na kiutendaji wa Jeshi letu ukizinduliwa rasmi kwa uzinduzi wa Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu. Sasa majukumu na mamlaka ya kiutendaji ya Jeshi letu lote yamepangwa kwa Kamandi. Pamoja na Kamandi hii tunayo Kamandi ya Jeshi la Anga na Kamandi ya Jeshi la Majini.
Kama mtakavyokumbuka, mapema miaka ya 80 tulikuwa na Kamandi mbili tu, yaani ya Ulinzi wa Anga na ya Wanamaji. Shughuli nyingine zote za Jeshi ambazo sasa tumezindua Kamandi yake ya Nchi Kavu, yaani Vikosi, Brigedi na wakati ule Divisheni za askari wa miguu zilikuwa zinafanywa Makao Makuu ya Jeshi. Kamandi mpya ya Jeshi la Nchi Kavu sasa ndiyo yenye jukumu la uongozi na usimamizi wa shughuli za kiutawala na kiutendaji za siku kwa siku za vikosi na brigedi. Makao Makuu ya Jeshi sasa yanabakia na majukumu ya msingi yanayohusu Jeshi zima ya sera, mikakati, na uratibu. Makao Makuu ya Jeshi yanahusika pia na masuala ya uwezeshaji wa Kamandi zake tatu na maslahi ya Wanajeshi kwa ujumla ili waweze kutimiza ipasavyo wajibu wao.
Nakupongeza sana CDF kwa uamuzi wako wa busara wa kufanya mabadiliko katika muundo wa Jeshi letu. Ni mabadiliko yanayoenda na wakati. Ndiyo maana sikusita kiyaunga mkono na kuyakubali. Nafarijika sana ninapoona Jeshi letu likijitahidi kuendeleza msukumo wa historia yake ya kubadilika kuendana na mabadiliko ya nyakati. Hiyo ndiyo siri kubwa ya uimara na mafanikio ya Jeshi letu.
Tangu Jeshi letu lianziswe mwaka 1964, limeshafanya mabadiliko mengi, ya kimuundo na kiutendaji kama matakwa ya kimazingira, kiutendaji na kiteknolojia yalivyojitokeza. Uzinduzi wa Kamandi hii unadhihirisha dhamira ya Jeshi letu ya kwenda na wakati. Mimi naamini ni mabadiliko yenye maslahi kwa Jeshi letu. Yatakaleta ufanisi na kuliimarisha Jeshi letu kwa utendaji kivita na kiutawala. Nawashukuru sana viongozi wa Jeshi na Wizara. Naomba muendelee kuwa wabunifu ili muendelee kufanya mabadiliko stahiki zaidi kwa nia ya kupata ufanisi mkubwa zaidi. Nasema tena hongereni sana.
Mheshimiwa Waziri, CDF, Makamanda na Askari;
Kuundwa kwa Kamandi hii, kunaleta uwiano wa kiutendaji kati ya Kamandi hii na Kamandi nyingine za Jeshi la Anga na Jeshi la Majini, hivyo kuongeza ufanisi katika utendaji wa Jeshi letu. Muundo huu pia, utasaidia kuleta ulinganifu wa mifumo ya Jeshi letu na majeshi ya nchi nyingine jirani katika jumuiya ya Afrika Mashariki na SADC na hata mataifa mengine rafiki duniani ambayo tunashirikiana nayo kwa mambo mbalimbali kama vile mazoezi na operesheni za pamoja. Hii itawasaidia wanajeshi wetu kushiriki kwa ufanisi zaidi kwenye mashirikiano hayo.
Ndugu Makamanda na Askari;
Wakati tunazindua Kamandi hii na kupongezana napenda kuwaomba muendelee kuwa wabunifu, mfikirie na kufanya mabadiliko zaidi yanayostahili ili muendelee kujiimarisha na kwenda na wakati. Ni muhimu kwa ajili hiyo mkaangalia miundo ya utumishi wa Jeshi, ikama, mitaala ya ufundishaji, zana na vifaa mbalimbali vya kijeshi ili navyo viendane na wakati. Napenda kuwahakikisheni kuwa Serikali itaendelea kuwaunga mkono katika jitihada zenu kadiri uwezo wa bajeti yetu utakavyoruhusu. Kwa moyo huo huo wa kuendelea kuwaunga mkono ndiyo maana nimekubali kuongeza umri wa kustaafu wa wanajeshi nchini kuwa miaka 60 badala ya 57 ya sasa. Mabadiliko hayo yatakayoanza Julai Mosi mwaka huu tunayafanya ili yaendane na wakati. Siku hizi watu wanachelewa kuzeeka tofauti na ilivyokuwa zamani,
Mheshimiwa Waziri; Naibu Waziri;
CDF, Makanda na Askari;
Nitakuwa mwizi wa fadhila kama sitaitumia nafasi hii, kwa mara nyingine kuwapongeza Wanajeshi wetu wote kwa kazi nzuri mnayoifanya ya kulinda uhuru na mipaka ya nchi yetu. Septemba Mosi, mwaka huu JWTZ litatimiza miaka 45 tangu kuasisiwa kwake. Imekuwa ni miaka 45 ya utumishi uliotukuka na mafanikio makubwa. Jeshi letu limetekeleza majukumu yake kwa ushujaa, umahiri, utii na uaminifu wa hali ya juu. Jeshi letu limezingatia kwa dhati misingi ya uweledi na uzalendo. Matokeo yake ni usalama na utulivu endelevu wa nchi yetu na watu wake. Tumefanikiwa kulinda mipaka ya nchi yetu wakati wote hata pale palipotokea tishio la wazi la nchi kuvamiwa na sehemu kutekwa na majeshi ya fashisti Idd Amin wa Uganda mwaka 1978. Nakumbuka Operesheni CHAKAZA mwaka 1978 – 1979. Nawapongeza sana.
Ndugu Makamanda na Askari;
Leo tunapozindua Kamandi hii, ninayo imani kubwa kwamba Jeshi letu litaendelea kujengeka na kwamba tutegemee mafanikio makubwa zaidi siku za usoni. Jeshi letu linaimarika zaidi na hivyo litaweza kutimiza vizuri zaidi jukumu lake la msingi la kulinda mipaka ya nchi yetu. Uimara utokao ogopesha wajinga wa nje na ndani kutothubutu kuchezea uhuru na mipaka ya nchi yetu. Jeshi letu pia litaendelea kutimiza ipasavyo wajibu wake wa kimataifa. JWTZ nao uzoefu wa kutosha na uweledi mkubwa katika nyanja za kimataifa. Limeshashiriki kwa ufanisi mkubwa katika operesheni nyingi, ndani na nje ya nchi. JWTZ limefundisha wapigania uhuru wa nchi za Kusini mwa Afrika wakati wa vita vya ukombozi. Sasa linaendekea kutoa mafunzo kwa wanajeshi wa nchi rafiki. JWTZ limeshiriki katika harakati na vita vya ukombozi na kuhami nchi marafiki.
Nazikumbuka operesheni KUMEKUCHA dhidi ya Wareno 1960, TEGAMA – Msumbiji, dhidi ya majeshi ya Rhodesia na Afrika Kusini, (1975 – 1980); SAFISHA – Msumbiji, dhidi ya RENAMO (1986 – 1988); Operesheni dhidi ya Mamluki waliovamia kisiwa cha Shelisheli mwaka (1981 – 1982) na hivi karibuni operesehni DEMOKRASIA huko Comoro mwezi Machi hadi Aprili, 2008 ya kumuondoa Kanali muasi Mohamed Bakar kutoka kisiwa cha Anjuan. Jeshi letu pia limekuwa linashiriki katika operesheni za kulinda amani chini ya Majeshi ya Umoja wa Mataifa. Hivi sasa tunajiandaa kwenda Darfur kwa ajili hiyo. JWTZ lina hazina kubwa ya uzoefu kutokana na operesheni hizo.
Ndugu Makamamanda na Wapiganaji;
Naomba nimalize kwa kuwashukuru tena, kwa kazi nzuri mnayoendelea kuifanya ya kulinda nchi yetu. Napenda kuwahakikishia kwamba Serikali inawajali na inathamini kazi yenu. Nawaomba msisahau kuwa siri kubwa ya mafaniko yetu Jeshini ni: Umoja, Ujasiri, Nidhamu na Uweledi. Yazingatieni. Nawatakia kila kheri katika majukumu yenu.
Asanteni sana.

Tuesday, 3 March 2009

Upimaji Ardhi TZ

Wananchi waanza kupimiwa ardhi

Serikali imeanza kuchukua hatua ya kurasimisha ardhi na nyumba za wakulima na wafugaji ili kuwawezesha kupata mikopo benki, mifuko na taasisi za fedha nchini ili kuwaondoa katika umaskini uliokithiri.

Kauli hiyo ilitolewa juzi na Waziri wa ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, John Chiligati wakati akizindua upimaji na utoaji wa hati miliki za ardhi kimila uliofanyika Wilaya ya Bariadi mkoani Shinyanga.

Wilaya hiyo ni moja ya maeneo ya majaribio kitaifa. Nyingine ni ya Babati mkoani Arusha pia.

Uzinduzi huo wa mpango umefanyika baada ya viongozi wa serikali na vyama vya kisiasa na wataalamu kupewa mafunzo elekezi wilayani humo ya kuchambua chimbuko la mradi huo katika utekelezaji wa sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995 na Sheria ya Ardhi ya Vijiji namba 5 ya mwaka 2004.

Chiligati alisema hatua hiyo ni ya utekelezaji wa Mkakati wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara Tanzania (Mkurabita) kwa lengo la kuwawezesha Watanzania kurasimisha ardhi na nyumba zao ili waweze kuzitumia kupata mikopo kwa urahisi.

Alisema mpango huo ambao ni wa kwanza kutekelezwa nchini utawawezesha wakulima na wafugaji kumiliki ardhi zao za kimila kwa kuhusisha serikali za vijiji na kupanga matumizi bora ya ardhi.

Alisema maeneo muhimu ambayo yatazingatiwa wakati wa upimaji huo ni ya makazi, huduma za kijamii, makaburi na maeneo ya hifadhi ya ardhi ya kijiji kama vile maeneo ya malisho.

Alisema baada ya kutambua kila kipande cha ardhi ndani ya kijiji chini ya mpango huo, ndipo utekelezaji utafanyika kwa kutambua mipaka ya kila mwenye shamba au eneo la malisho ya mifugo na kuweka mipaka bayana.

Pamoja na kuweka kumbukumbu za miliki ya ardhi bayana, alisema mpango huo pia utammilikisha na kumpatia kila mhusika hatimiliki ya eneo lake, wakati kipande cha ardhi kwa mtu mmoja mmoja au familia ya mume na mke au eneo linalomilikiwa kiukoo itamilikishwa kwa kupitia kiongozi wa familia au ukoo.

Chiligati aliagiza kuwapo kwa ushirikishwaji wa kila mwanakijiji na kuutaja mradi huo kuwa ni shirikishi.



SOURCE: Nipashe, 2009-03-03 10:55:06
Na Stephen Wang`anyi, Shinyanga